Header Ads

WAHITIMU WA CHUO CHA UANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUWA KIOO CHA JAMII

Na Paschal D.Lucas wa TAEATI.
      Chuo cha The Arusha East African Training institute kilichopo Philips Arusha mjini kimepongezwa kwa kufanya vizuri katika matokeo na kutoa waandishi na watangazaji bora katika vyombo mbalimbali vya habari nchini.
       Akizungumza katika sherehe ya mafahali iliyofanyika Disemba 8, 2017 katika viwanja vya chuo hicho mgeni rasmi ambaye alimwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Arusha mjini Bi.Rebeca Mathias ambaye ni Afisa Kilimo na Mifugo wa Mkoa wa Arusha aliupongeza uongozi wa chuo kwa kuendeleza vipaji na kutoa elimu iliyo bora kwa vijana hapa nchini katika tasnia ya habari na kuahidi kuwa atakuwa balozi wa chuo hicho.
       Bi.Rebeca Mathias aliongeza kuwa vijana waliohitimu wakawe kioo cha jamii kupitia elimu na mafunzo waliyoyapata wakiwa chuoni hapo kwa kufuata maadili ya taaluma yao na kuwa mabalozi namba moja wa chuo.
       Naye Mkurugenzi wa chuo hicho cha The Arusha East African Training institute Bw.Tilly Chizenga alimshukuru Bi.Rebeca Mathias kwa kukubali kufika kushiriki sherehe za mahafali chuoni hapo na wote walioshiriki kufanya maandalizi wakiwemo wazazi na walezi kwa ujumla.
       Aidha Bw.Tilly Chizenga alieleza mbele ya mgeni rasmi kuwa chuo hicho kina ufinyu wa eneo la kujifunzia na kumwomba mgeni rasmi afikishe ombi na kuishauri serikali kupitia Mkuu wa mkoa na Mkuu wa Wilaya kuwa Serikali iweke mpango wa mkopo wa kifedha hata kwa wanaosoma elimu ya chini au wafadhili ili wamudu malipo ya ada wakiwa chuoni ili kuongeza ufanisi na idadi ya vijana wanaotoka familia zisizo na uwezo mkubwa wa kifedha ili kumudu malipo wawapo chuoni.

No comments