Header Ads

Wema Sepetu akabaki huko huko CHADEMA ama akaanzie kwenye shina

polepole
Katika kujenga nidhamu ya chama, na kuepuka kukifanya chama daladala kwamba unapanda na kushuka wakati unaotaka, kuna taratibu za kufuatwa mtu anapotaka kujiunga na chama, na sio kutangaza mitandaoni.
Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo ni muda mfupi tu baada ya muigizaji wa filamu nchini, Wema Sepetu kutangaza kuwa ameamua kurejea Chama cha Mapinduzi CCM.

“Nimesikia habari mitandaoni, napenda kuweka rekodi sawa, chama chetu sio daladala ambayo mtu anaweza panda na kushuka wakati wote apendao. Chama chetu kina misingi, imani, masharti ya uanachama, na zaidi ya yote ahadi ya mwanachama ambayo ni moja inasema, Nitakuwa Mwananchama mwaminifu wa CCM.”
Aidha, Polepole amesema kwamba, ni heri Wema Sepetu akabaki huko huko (CHADEMA) ama akaanzie kwenye shina la chama ambapo ndipo alipochukulia kadi kabla ya kuhama.
“…kukosa uaminifu kwa chama inatosha kumkataa mtu kuwa mwanachama wetu,” aliandika Polepole akisema kwamba katika kuijenga CCM mpya sio kazi ndogo na kwamba inahitaji viongozi wanyenyekevu na watumishi na wanachama waaminifu.
Mapema jana jioni, Wema Sepetu alitangaza kujiengua CHADEMA na kurejea CCM akidai kuwa, hawezi kuendelea kuishi kwenye nyumba inayomkosesha amani, kwani kwake yeye utulivu wa akili ni kila kitu.

No comments