WANACHUO WAHIMIZWA KUWA KIOO CHA JAMII
Na Paschal D.Lucas
Katika kusherekea mahafali ya chuo kikuu cha Tumaini Makumira kilichopo Usa River Arusha mkuu wa chuo hicho cha Tumaini Makumira Dkt.Askofu.Fredrick Shoo ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo yaliyofanyika leo Disemba 2,2017 katika viwanja vya chuo hicho.
Akihutubia maelfu ya wageni na wahitimu waliokuwapo kwenye Mahafali hiyo Dkt.Askofu Fredrick Shoo amewatunuku vyeti wahitimu wote waliosoma chuoni hapo kwa ngazi zote wapatao 842 na kuwataka wahitimu hao wakawe kioo na dira kwa jamii kupitia mafunzo na elimu walioipata pindi wakiwa chuoni hapo.
Naye Dkt.Faustine Mahali ambaye pia ni Makamu mkuu wa chuo hicho akiongea kwa niaba ya Prof. Ismail R. Mbise amewataka wahitimu hao kuwa waajibikaji na watu wakujituma ili kuleta ufanisi katika shughuli na maendeleo ya taifa kwa ujumla kupitia maarifa waliyovuna wakiwa chuoni hapo.
Picha ya wahitimu wakimsikiliza Mgeni rasmi Dkt.Ask. Fredrick Shoo
Wahitimu wa chuo cha Tumaini Makumira wakifurahia jambo wakati wa mahafali
Picha na Paschal D.Lucas
No comments