Header Ads

BABU SEYA AKUTANA NA RAIS IKULU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 02 Januari 2018 amekutana na Mwanamuziki Nguza Viking na watoto wake waliofika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa lengo la kumshukuru kwa kupatiwa msamaha wa kuachiwa huru kwake Nguza Viking (Babu Seya) na Mwanae Papii Nguza (Papii Kocha) waliokuwa wakitumia adhabu ya kifungo cha maisha jela.Nguza Viking na Papii Nguza wakiwa na wana familia wengine Nguza Mbangu na Francis Nguza wamezungumza na Mhe. Rais Magufuli ambapo wamemshukuru kwa msamaha alioutoa kwao na kwa wafungwa wengine 61 waliokuwa wamehukumiwa adhabu ya kifo, na wamemuahidi kuwa raia wema na watachapa kazi kwa juhudi na maarifa.“Yaani sijui nisemaje, hapa nina furaha kubwa sana moyoni mwangu, nilikuwa naomba sana tangu muda mrefu nikutane nae, nimeomba sana sana, hatimaye leo nimefanikiwa na nimemwambia namshukuru sana kwa kutusamehe na sasa nipo tayari kuchapa kazi, Hapa Kazi Tu” amesema Nguza Viking na kuungwa mkono na mwanae Papii Nguza.Nguza Viking na wanae wamemuombea Mhe. Rais Magufuli na wameiombea nchi, na pia msemaji wa familia hii Nguza Mbangu amesema wanajipanga kuendeleza kazi zao za sanaa.Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amewashukuru kwa kuja kumuona na kumshukuru lakini amesema shukrani zimwendee Mwenyezi Mungu ambaye ndiye husamehe.

No comments