TCRA YAZIPIGA FAINI VITUO VITANO VYA RUNINGA
Mamlaka ya mawasiliano Tanzania, TCRA, imevipiga faini vituo vitano vya Televisheni kwa makosa ya ukiukwaji wa taratibu za kutangaza taarifa ya habari hapa nchini.Adhabu hiyo imetangazwa leo na Makamu mwenyekiti wa kamati ya Maudhui ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) , Joseph MapundaKituo cha runinga cha EATV, kimetozwa faini ya jumla ya TZS milioni 15, kwa makosa matatu ikiwemo, kukiuka maadili ya uandishi na kutangaza habari za uchochezi. Faini hiyo inapaswa kulipwa ndani ya siku 30, na kituo hicho kitawekwa chini ya uangalizi kwa muda wa miezi 6.Aidha, TCRA imekitoza faini ya TZS milioni 15 kituo cha Runinga cha Channel ten, kwa makosa ya kutangaza habari ambazo hazikuzingatia maadili ya uandishi, kutangaza habari za uchochezi, na kutozingatia mizania. Pia kituo hicho kitawekwa chini ya uangalizi kwa miezi sita kuanzia leo.Kituo cha runinga cha Star TV, kimetozwa faini ya jumla ya TZS milioni 7.5 kwa makosa matatu ikiwemo, kukiuka maadili ya uandishi na kutangaza habari za uchochezi. Faini hiyo inapaswa kulipwa ndani ya siku 30 na pia kituo hicho kinawekwa chini ya uangalizi wa miezi 6.Pia TCRA imekitoza faini ya TZS milioni 7.5 kituo cha runinga cha Azam Two, kwa makosa ya kutangaza habari za uchochezi, kutangaza habari ambazo hazikuzingatia maadili ya uandishi na kutozingatia mizania. Pia kituo hicho kitawekwa chini ya uangalizi kwa miezi sita kuanzia leo. Kituo cha runinga cha ITV, kimetozwa faini ya jumla ya TZS milioni 15, kwa makosa matatu ikiwemo, kukiuka maadili ya uandishi na kutangaza habari za uchochezi. Faini hiyo inapaswa kulipwa ndani ya siku 30, na kituo hicho kitawekwa chini ya uangalizi kwa muda wa miezi 6.
No comments