Header Ads

BOKO HARAM WACHOMA KIJIJI

Kutoka Nigeria kundi lenye itikadi kali za Kiislam la Boko Haram,jana limechoma kijiji kizima kilichoko Kaskazini Mashariki mwa nchi ya Nigeria,na kuua watu wawili kwa kuwachoma wakiwa hai.kwa mujibu wa Shirika la habari la AFP,lililowakariri baadhi ya wananchi,na vyanzo vya usalama,Boko Haram,limetekeleza shambulizi hilo katika kijiji cha Alau-Kofa, takribani kilometa 12 sawa na maili 7.5 kutoka mji mkuu wa jimbo la Maiduguri,ambao ni makao makuu ya jimbo la Borno.
AFP limedai kuwa kundi hilo limetumia silaha mbalimbali kukiangamiza kijiji hicho ikiwemo maguruneti,na maroketi ambapo shambulio hilo limeharibu makazi ya wananchi hao.

No comments