Header Ads

VYUO KUENDELEA KUFUNGWA

Kutoja Bungeni Dodoma serikali imeendelea kudhibiti ubora wa elimu nchini kwa kuvichukulia hatua vyuo na shule zinazobainika kukiuka taratibu za utoaji wa elimu ikiwa ni pamoja na kusitisha udahili wa wanafunzi,kusitisha program zitolewazo,kupunguza idadi ya wanafunzi waliozidi na kufuta usajili wa taasisi husika.
    Katika Mwaka 2017/18 ulifanyika uhakiki katika vyuo na taasisi 458 za elimu ya ufundi ambapo jumla ya vyuo na taasisi 59 zilibainika kuwa na mapungufu na hivyo walitakiwa kurekebisha mapungufu hayo ndani ya kipindi cha miezi mitatu kuanzia Februari 1 Mwaka 2018,chuo kitakachoshindwa kurekebisha mapungufu hayo kitafutiwa usajili.Kauli hiyo imetolewa jana  bungeni na Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,William OleNasha alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum,Zubeda Sakuru (Chadema),lililoulizwa kwa niaba yake  na Mbunge wa Viti Maalum,Susan Lymo.

No comments