Header Ads

WANAOTUHUMIWA NA KIFO CHA MSANII MOWZEY RADIO WAANZA KUKAMATWA.

     Baada ya kifo cha msanii Mowzey Radio wa Uganda polisi katika mji wa Katoe Uganda wamemkamata kijana Godfrey Wamala mmoja kati ya watuhumiwa waliohusika na shambulio la mwili lililopelekea kifo cha msanii Mowzey Radio.
     Kijana Wamara mwenye umri wa miaka 28 alikamatwa akiwa Kyengera ilikodaiwa alijificha nyumbani kwa rafiki yake kwa siku kadhaa baada ya tukio la shambulio la msanii Mowzey.
     Wamara amepelekwa katika mji wa Entebbe ambapo polisi wanatarajia kumfungulia mashtaka ya mauaji ya msanii Mowzey.

No comments