DR.SHEIN KULIPA MADAI YA WAALIMU ZANZIBAR
Ikiwa serikali ya Tanzania bara ikikamilisha uamzi wa kulipa malimbikizo ya wafanyakazi na watumishi wa umma wakiwemo na waalimu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohammed Shein amesema sera ya elimu bure kwa wanafunzi wa sekondari itaanza ifikapo mwezi june mwaka huu.
Amesema hayo wakati akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Sita wa chama cha walimu Zanzibar amesema serikali imeamua kuondoa ada kwa wanafunzi kwa lengo la kuendeleza sera ya rais wa awamu ya kwanza Shekh Abeid Amani Karume.
Amesema sera ya elimu bure itaimarika endapo walimu watafanya kazi kwa mujibu wa sheria na maendeleo ya elimu yatajengeka iwapo walimu watakuwa na juhudi na uimara pamoja na misingi bora na zamira njema ya kufundisha wanafunzi mashuleni.
Dr. shein amesema anatambua matatizo yanayowakabili walimu yakiwemo uhaba wa walimu, uchache wa vifaa vya kufundishia pamoja na malimbikizo ya madeni ya mishahara ya walimu .Hivyo ameiagiza wizara ya elimu kuhakikisha wanawalipa madeni yote wanayodai walimu kabla ya kufikia mwaka 2019 kwani kuendeleza deni hilo litapunguza ari ya ufundishaji kwa walimu na kupelekea sekta ya elimu kushuka kutokana na maslahi madogo ya walimu.
Hata hivyo Rais Shein amesema ameridhishwa na matokeo yaliyopatikana katika mitihani ya taifa kwa elimu ya msingi na sekondari na kuitaka wizara ya elimu kukaa pamoja na shule zote za Zanzibar zile zilizofanya vibaya katika mitihani ya taifa ili kuweza kujua sababu zilizopelekea kufeli kwao kwenye mitihani hiyo.
Aidha amesema serikali itaendelea kujali na kuthamini michango ya walimu yanayotoka katika taifa kwa kujali maslahi yao.
Akisoma risala ya walimu Katibu Mkuu wa chama cha walimu Zanzibar Mussa Omar Tafurwa amesema miongoni mwa matatizo yanayowakabili ni tatizo la uhaba wa walimu kwa shule za Pemba, mikoa ya Kaskazini na Kusini kwa Unguja.
Tafurwa ameiyomba serikali kufanya uwekezaji wa rasilimali fedha ya kutosha ili kuweza kuajiri walimu ,kununulia vifaa vya kufundishia pamoja na kulipa madeni ya walimu wanayodai kwani pia baadhi yao wamesha staafu na wengine wamekwishafariki.
Amesema pia licha ya matatizo hayo pia walimu wanakabiliwa na mazingira magumu ya kufundishia ambapo hupelekea kuumwa na kushindwa kufanya kazi vizuri hivyo wameiyomba serikali kuwaanzishia bima ya afya kwani wanashindwa mukumu gharama za matibabu kwani fedha wanayoipata bado haikidhi haja.
No comments