HABARI PICHA: MAZISHI YA KIGUNGE ULIVYOKUTANISHA VIONGOZI
Februari 5, 2018 ilikuwa siku ya mazishi ya mzee mkongwe nchini Tanzania Marehemu Kingunge Ngombale Mwiru.
Mazishi hayo yalikutanisha viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Dk.John Pombe Magufuli na marais wengine wastaafu wa Tanzania.
Pia katika mazishi hayo yaliyofanyika katika makaburi ya Kinondoni alikuwepo pia Mama Maria Nyerere.
Hapa nimekusogezea picha za matukio yaliyojili siku ya mazishi.
Rais wa awamu ya tatu Benjamin W.Mkapa akiweka shada la Maua kwenye kaburi la Marehemu Kigunge N.Mwiru kwenye makaburi ya Kinondoni.
Baadhi ya wanafamilia na waombolezaji wakati wa mazishi ya Mzee Kigunge N. Mwiru
Jeneza la mwili likiwa limewekwa tayari kaburini kwa ajili ya maziko.
Viongozi wa serikali wakiwa wamezunguka kaburi la Mzee Kigunge
Rais wa Dk.John Pombe Magufuli akisalimia na baadhi ya waombolezaji.
Kiongozi wa dini akiwa ananyunyuzia maji ya baraka Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Mzee Kingunge Ngombale Mwiru
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli akiweka mchanga kwenye kaburi wakati wa mazishi.
Rais wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk.John Pombe Magufuli akiweka shada la Maua kwenye kaburi la Marehemu Kingunge hapo jana kwenye makaburi ya Kinondoni.
No comments