Header Ads

MKURUGENZI AAGIZA MALIPO YA POSHO ZA MADIWANI ZIELEKEZWE KWENYE KUBORESHA MIUNDOMBINU YA SHULE NDANI YA HALMASHAURI YA ARUSHA DC

 
 Tukiwa bado na mwaka wa Fedha 2017/2018 Halmashauri nyingi nchini zikipiga hatua kwa kujadiliana mipango mbalimbali ya maendeleo ndani ya vikao vya Halmashauri kwa kushirikiana na madiwani lakini haikuwa hivyo kwa Halmashauri ya wilaya ya Arusha DC ambapo Februari 8, 2018 kulitokea kutokuelewana na migongano ya kimasilahi baina ya madiwani wa Ccm na Chadema huku Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Wilson Maheka kuamua kuchukua maamuzi ya kiutendaji.
   Maamuzi hayo ya Mkurugenzi yalitokana na madiwani wa Chadema wakiongozwa na mwenyekiti wa Baraza la madiwani Bw.Noah Lebris (Chadema) kutokuhudhuria kikao cha kujadili Maendeleo ya halmashauri hiyo pamoja na kuapishwa kwa Diwani wa Kata ya Musa Bi.Flora Zelothe aliyeshinda katika changuzi ndogo iliyofanyika kata ya Musa ndani ya halmashauri ya Arusha.
   Kutokuhudhuria kikao kwa madiwani wa Chadema kulimlazimu mkurugenzi wa halmashauri hiyo kulaumu na kukilaani kitendo hicho na kumlazimu kuelekeza pesa zilizokuwa zimeandaliwa kwa ajili ya malipo ya kikao hicho zaidi ya Milioni nane kuzipeleka kwenye uboreshaji wa miundombinu kwa shule za msingi ndani ya halmashauri ya Arusha DC.
    Kitendo hicho kiliwakera madiwani wengi ambapo Diwani wa viti Maalum Bi.Yasmin Bachu naye alisema kuwa kitendo cha madiwani wa Chadema kukataa kuhudhuria kikao hicho kimemsikitisha sana na kuwa suala la malipo ya posho ni la madiwani wote hivyo kutokuhudhuria kikao kunakwamisha Maendeleo ya halmashauri na uboreshaji wa huduma za kijamii ndani ya halmashauri.
"Kwa kuwa lengo la kikao hiki ni kujadili na kupitisha baheti mbalimbali za kiutendaji ndani ya halmashauri yetu hivyo tabia hii haivumiliki na tuko tayari hata baraza hili livunjwe kwani timu nzima ya mkutugenzi na Wataalamu wake wanaweza kufanya kazi tunazofanya madiwani" Alisema Bi.Yasmin Bachu.
   Naye diwani wa kata ya Shambasha Bw.Lengai Olesabaya  hakupendezwa na kitendo hicho cha madiwani wa Chadema wa chadema cha kususia kikao na kuunga mkono wazo la Bi.Yasmin Bachu la kuvunja baraza hilo na kudai kuwa madiwani wa Chadema wamekuwa wakwamishaji  na kusababisha ilani ya ya chama cha mapinduzi kutotekelezwa kwa wananchi hivyo madiwani wa chadema wamekuwa wakiyapa kipaumbele maslahi yao binafsi kuliko kero na shida za wananchi waliowapa ridhaa ya kuwawakilisha na kuwataka waachane na hizo tabia.
   Kufuatia agizo lake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Arusha DC Bw . Wilson Mahela zaidi ya shilingi milion 14 zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya malipo ya madai ya  posho za madiwani kwa vikao viwili pesa hizo hazitalipwa kwa sasa  hadi mwezi Machi.Na kuongezea kuwa zaidi ya Shilingi milioni140 zinatakiwa kwenda kwenye miradi ya kata ndani ya Halmashauri kwa ajili ya maendeleo na uboreshaji wa miundombinu.
    Baada ya kusema hayo Bw . Wilson Mahela alimwomba mwanasheri  wa Halmashauri hiyo Bw. Dostan Shimbo kusoma vifungu vya sheria na kutoa mwongozo na kumuapisha diwani mteule Bi.Flora Zelothe na mara baada ya kumwapisha diwani huyo kikao kiliahirishwa kwa sababu ya idadi ndogo wa wajumbe hivyo wasingeweza kuendelea na kikao hicho.
   Akijibu tuhuma za kususi kikao hicho mbele ya waandishi wa habari  mwenyekiti wa baraza hilo la madiwani Bw.Noah Lebris ( Chadema ) alidai kuwa sababu za kutokuhudhuria kikao hicho ni idadi ndogo ya madiwani waliohudhuria kwa mujibu wa kifungu cha sheria iliyotokana na udhuru kwa baadhi ya madiwani kwenda misibani kwenye maeneo yao na akakanusha taarifa za kususia kikao kwa sababu ya posho.

No comments