MWANZA: ATIWA MBARONI KWA KUMBAKA MTOTO WA MIAKA MINNE
Jeshi la Polisi mkoani Mwanza, linamshikilia mkazi mmoja wa kata ya Nyegezi Wilaya ya Nyamagana kwa tuhuma za kumnajisi mtoto wa miaka minne (jina limehifadhiwa) na kumsababishia majeraha na maumivu makali katika sehemu za siri Februari 26, 2018.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna Ahmed Msangi, katika taarifa aliyoitoa jana kwa vyombo vya habari, alisema mtuhumiwa alitenda kosa hilo juzi majira ya saa 10 jioni katika maeneo ya mtaa wa Password kata ya Nyegezi, Nyamagana mkoani hapa.
Inadaiwa kuwa mtoto huyo alikuwa akicheza nje na wenzake ndipo mtuhumiwa alimwita na kwenda naye chumbani na baadaye mtuhumiwa alifanyia mtoto ukatili kwa kumbaka na kumsababishia maumivu makali katika sehemu za siri.
Baada ya kunfanyia ukatili huo mtuhumiwa alimwonya mtoto ake kimya asimwambie mtu yeyote juu ya jambo hilo.Msangi alisema baada ya mtoto kufanyiwa ukatili huo, alikaa kimya bila kumwambia mtu yeyote hadi mama yake aliporejea kutoka kazini.
Kamanda Msangi alisema wakati mama yake akienda kumwogesha, ndipo alipogundua kuwa mtoto amefanyiwa ukatili huo kisha alitoa taarifa kituo cha polisi.
Mara baada ya kutoa taarifa, polisi walifanya ufuatiliaji wa haraka hadi eneo la tukio na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa.
Kamanda Msangi alisema polisi wako katika upelelezi na mahojiano na mtuhumiwa na kwamba uchunguzi ukikamilika, mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kwa hatua zaidi stahiki za kisheria.
Kamanda Msangi alisema mtoto huyo alipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Nyamagana na kwamba hali yake inaendelea vizuri.
Kamanda Msangi ametoa wito kwa wananchi wa mkoa wa Mwanza hususani wazazi kuwa waangalifu kwa mtoto dhidi ya watu eenye nia mbaya na kusisitiza kuwa waache kwa watu wazima kwa ajili ya kuwaangalia na kusimamia usalama wao pindi waendapo kazini.
No comments