Header Ads

Netanyahu aishambulia Iran akiita "chui milia hatari"


Netanyahu brandishes Iranian drone fragment
Waziri mkuu wa Israel ameishambulia vikali Iran akiuambia mkutano wa ulinzi huko Munich kuwa Iranana tisho kubwa kwa dunia yetu.
Benjamin Netanyahu alisema kuwa "Israel haitaruhusu Iran kuiweka kamba ya ugaidi kwenye shingo lake.
Bw Netanyahu alifananisha makubaliano ya Munich ya mwaka 1938 yaliyoonekana kama jitihada zilizofeli za kuifurahisha Ujerumani ya Nazi na makubaliano ya nyuklia ya Iran ya mwaka 2015
Alisema makubaliano hayo "yaliwachilia chui milia hatari ambayo ni Iran".
Alisema kuwa Iran inadanganya kuwa haikutuma ndege isiyo na rubani kwenda Israeli wiki iliyopita ambayo ilidunguliwa na jeshi la Israel.
Akishika kifaa cha kile alichokitaja kuwa mabaki ya ndege isiyo na rubani iliyodunguliwa, Netanyahu alimwambia moja kwa moja mjumbe wa Iran ambaye ni waziri wa mashauri ya nchi za kigeni, akimwambia: "Unatambua hiki, unastahili, ni chenu, msitujaribu."

No comments