SERIKALI KUANZA UKAGUZI WA MAGARI YA WATU BINAFSI
Naibu Waziri wa Mambo ya ndani amesema leo kuwa ifikapo tarehe 1 Machi, 2018 kutaanza ukaguzi wa magari binafsi nchi nzima na kila gari litalipia stika ya ukaguzi ambayo gharama yake ni Shilingi elfu tatu ili kujiridhisha kama limekaguliwa.
Ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wanahabari, Mh. Masauni amesema kuwa Wamiliki wa magari madogo wanatakiwa kupeleka magari yao katika vituo vya polisi ili kuyafanyia ukaguzi kama yanastahuili kuendelea kukimbia barabarani.Aidha Mh. Masauni amewaonya maaskari kuhusu zoezi hilo kwa kuwaambia kuwa "Askari yoyote atakayetumia nafasi yake kutoa stika ya gari bila kulifanyia ukaguzi na ilihali halina vigezo vya kupewa stika nataka niwaambie kuwa huu si wakati wake, zama zimebadilika". Mh. Masauni ameongeza kwamba "Nataka madereva wa pikipiki ambazo zitakamatwa na kukutwa zimesajiliwa kwa majina ya kampuni badala ya majina binafsi wachukuliwe hatua mara moja".
Naye Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania, Fortunatus Musilimu amesema katika ukaguzi wa magari madogo utakaoanza mwezi Machi, mtu atakaekiuka na kukataa kupeleka gari lake kufanyiwa ukaguzi atakamatwa na sheria itachukua mkondo wake kufuatia kukiuka agizo la serikali.
No comments