Header Ads

WAZEE KUHUDUMIWA NA RIBOTI NCHINI JAPAN

Serikali ya Japan imeamua kuwa roboti zitatumika kutoa huduma kwa asilimia 80 ya wazee nchini humo mpaka kufikia mwaka 2020.
Gazeti  la "The Guardian" limechapisha habari ya kuwa kiwanda cha roboti nchini Japan kina mpango wa kuboresha roboti ili kurahisisha maisha ya wazee nchini humo kwa kutumia teknolojia.
Roboti hizo zitakuwa zikiwasaidia wazee kwa kuwatoa kwenye vitanda hadi kwenye viti vyao na vilevile kuwasaidia kwenye kuoga.
Dr Hirohisa Hirukawa
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Robot, Taasisi ya Taifa ya Sayansi ya Juu na Teknolojia amesema kuwa lengo lake kuu ni kurahisisha maisha ya wazee walio katika vituo tofauti na vilevile waliopo majumbani.
Dr Hirohisa Hirukawa amesema kuwa ni asilimia nane ya vituo vya kulelea wazee vinatumia roboti katika kutoa huduma zake.

No comments