Header Ads

JAFFO ATOA MAAGIZO KWA MAAFISA HABARI NA MAKATIBU TAWALA KOTE NCHINI

Na.Paschal D.Lucas
paschaldlucas@gmail.com.
Arusha.
Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jaffo amewataka Maafisa habari wote nchini kutoa taarifa kwa wakati zinazohusu utendaji wa serikali ya awamu wa tano na kuongeza kuwa Afisa habari ambaye hatatosha kutimiza wajibu wake atamwondoa ofisini na kumpa mtu mwingine.
Ameyasema hayo leo Machi 16, 2018 wakati akifunga semina ya maafisa habari, mawasiliano na uhusiano serikalini ( TAGCO) kilichodumu kwa siku 5 katika Ukumbi wa jengo la AICC jijini Arusha.
Jaffo amewataka na kaagiza kuwa Halmashauri zote nchini kutenga bajeti ya ajili ya maafisa habari habari wa wilaya ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa wakati na kununua vifaa kama vile kompyuta na Camera.
Aidha amewaagiza makatibu tawala wote wa mikoa na wilaya nchini  kuwa wahakikishe kuwa maafisa habari wote wa Halmashauri zote wanaingia kwenye vikao vyote vya maamuzi vya halmashauri ili kuchukua taarifa sahihi za halmashauri husika.
Ikiwa Lengo la kikao hicho ni kikao  ni kubadilishana na mawazo na namna ya kutuma na kutoa taarifa kwa wananchi husika na lengo la mwanahabari wa kila halmashauri ni kuhakikisha wananchi wanapata taarifa ameagiza suala la takwimu kwa wakuu wa idara zote wahakikishe wanatoa kwa maafisa habari ili kuwezesha kutoa takwimu iliyo sahihi.
Kwa upande wa uwezeshwaji kwa maafisa habari amesema kuwa kwa kuwa mamlaka ya serikali za mtaa kwa halmashauri zote nchini  liko chini yake amemhakikishia Katibu mkuu wa idara ya Habari maelezo Dr.Hassan Abbas kuwa atalisimamia  mwenyewe.
Hata hivyo amewataka maafisa habari wote nchini kupitia kikao na semina hiyo kwa maafisa habari, mawasiliano na uhusiano ambacho hufanyika mara moja kwa kila mwaka waende wakabadilike katika utendaji wao wa kazi.
Kikao hicho kilichofanyika kwa siku tano kinatarajiwa kufanyika tena mwakani ambapo washiriki walipendekeza kifanyike jijini Mwanza.

No comments