Header Ads

RAIS KAGAME APIGA MARUFUKU VIPAZA SAUTI MISIKITINI

Kwa mujibu wa idhaa ya kiswahili ya Marekani (VOA) mamlaka jijini Kigali nchini Rwanda imepiga marufuku matumizi ya vipaza sauti vinavyotumika kutoa adhana kwenye misikiti.

Hatua hii imekuja wiki mbili baada ya mamlaka jijini Kigali kuyafunga makanisa zaidi ya mia saba. Pia baadhi ya makanisa yalifungwa kwa sababu ya kutokuwa na usajili.Kwa mujibu wa maelezo ya mshauri mkuu wa mufti wa Rwanda Sheikh Mbarushimana Suleiman taarifa hiyo imepokelewa na kilichopo sasa wameanza kuifanyia kazi.

Sheikh Suleiman amefafanua kuwa Kama vile yalivyofungwa makanisa zaidi ya mia saba wiki mbili zilizopita jijini kwa ajili ya kelele huenda hii ni ishara kwamba hata misikiti ikafutia endapo wenyewe watashindwa kuridhia agizo hilo.

Lakini kufuatia agizo lililotolewa na mamlaka ya tarafa ya Nyarugenge mjini Kigali ambalo ni moja ya eneo lenye waislamu wengi, inawezekana sasa sauti za adhana zisisikike kwa upeo wa juu.
Katibu mtendaji wa tarafa hiyo Havuguziga Charles amefafanua kwamba hatua hii imechukuliwa kwa sababu ya kelele zinazodaiwa kuwasumbua wananchi.

“Baada ya kutathmini tatizo la kelele zinazowasumbua wananchi wakati wa ibada makanisani iliamuliwa kwamba hata vile vipaza sauti vilivyoko juu ya misikiti ambavyo waislamu hutumia wakati wa ibada kwamba vikome.
Tuliwaomba viongozi wa misikiti kwamba watafute njia mbadala za kuwataarifu waumini wao saa za ibada bila kutumia vipaza sauti kwa sababu vinasababisha kelele.,” amesema Nyarugenge.

Hatua hii imejiri wiki mbili baada ya kufungwa makanisa zaidi ya mia saba jijini Kigali kwa tuhuma hizo huku hata baadhi ya wachungaji wakiendelea kuzuiliwa kwa shutuma za kukaidi agizo hilo.

No comments