RAIS WA MAURITIUS AMEJIUZULU
Mwanamke wa kwanza kuchaguliwa kama rais nchini Mauritius amejiuzulu kutokana na madai ya kujihusisha na rushwa.
Ameenah Gurib alichaguliwa kama rais wa Mauritius baada ya kushinda katika uchaguzi mkuu mwaka 2015.
Mwanasehria wake Yousouf Mohamed amesema kuwa Bi Ameenah amejiuzulu kwa ajili ya maslahi ya taifa lake.
Hata hivyo Gurib ameyakanusha madai ya rushwa dhidi yake.
Kujiuzulu kwa rais huyo kutatambuliwa rasmi 23 mwezi Machi.
Wiki iliyopita waziri mkuu wa Mauritius Pravind Jugnauth alitangaza kuwa rais anatarajia kujiuzulu lakini Gurib-Fakim alikanusha madai hayo.Ameenah Gurib-Fakim pia alikanusha mashtaka ya rushwa dhidi yake, akisema kwamba hakuchukua fedha au thamani kutoka kwa mtu yeyote au taasisi.
No comments