WANAWAKE 600 WAPATA MKOPO WA SHILINGI MILIONI 120 ARUSHA
Waziri ofisi ya waziri mkuu, sera,Bunge
kazi,ajira,vijana na walemavu Mh.Jenista Mhagama amewataka akina mama kutumia
vyema fursa hasa ya mikopo wanayoipata toka kwa viongozi wa serikali
Ameyasema hayo leo Machi 23,2018 katika ukumbi wa AICC Arusha
wakati akifungua zoezi la utoaji mikopo kwa akina mama 600 na kukabidhi mfano wa hundi ya shilingi milioni
120 kwa akina mama wajasiriamali wadogo wa jiji la Arusha pesa ambayo ilitokana
na marejesho ya mikopo ya vijana wa bodaboda jiji la Arusha.
Amewataka akina mama kutumia vyema fedha za mikopo
toka kwa viongozi serikali na wahisani wa maendeleo ikiwa ni pamoja na matumizi sahihi ya
fedha hizo wazipatazo kwa kuzielekeza sehemu iliyo sahihi
na si vinginevyo.
Ameongeza kuwa kwa kuwa serikali ya awamu ya tano
inakwenda pamoja na mabadiliko hivyo basi wanawake pia wanapaswa kwenda sambamba
na mabadiliko hayo ya kiuchumi kwa kuhakikisha kwa wanajiongeza katika suala la
kiuchumi kwa kujishughulisha na biashara ndogondogo zinazoweza kuwaingizia
kipato kupitia mikopo inayotolewa na viongozi mbalimbali pamoja na wahisani.
Aidha amewataka akina mama kurejesha fedha za mokopo
kwa wakati ili kupata fursa nyingine za
kimkopo na kuwajengea uaminifu kwa viongozi wa serikali wanaofanya jitihada za
kumkomboa mwanamke kiuchumi.
Kwa upande wake Naibu waziri wa wa Ofisi ya waziri
mkuu, sera,Bunge,,kazi,ajira,vijana na walemavu Mh.Anthony Mavunde amewataka akina maam hao kuptia
mpango huo wakabadilishe maisha yao.
“Nitafurahi
kuwaona akina mama wa Arusha kupitia mpango huu wa leo maisha yenu
yanabadilika, wanasema mwanadamu anaweza kuwa masikini muda mwingineni
kujitakia, kama mwenyezi mungu amekujalia maarifa,kakujalia uwezo wa kufanya
kazi ukapata uwezesho kama huu naamini
kabisa ni rahisi sana maisha yetu yanaenda kubadilika”.
Naye mkuu wa mkoa wa Arusha Bw.Mrisho Gambo amesema
kuwa kabla ya kutoa mkopo huo walianza kwa kutoa mafunzo kwa akina mama
kitarafa namna ya kutunza fedha na jinsi ya kufanya biashara zao na kuongeza
kuwa fedha hizo hazitatolewa mkono bali watawekewa kupitia akaunti zao za kibenki
ili kuwaongezea utamaduni na utaratibu kutunza fedha zao kupitia benki.
No comments