Header Ads

JUKUMU ZITO ALILILOPEWA KICHUYA

Baada ya kufanikiwa kuivuruga Singida United juzi, Mtibwa Sugar wamesisitiza kwamba hizo ni salamu tosha kwa Simba na kuwataka wajiandae kisaikolojia.

Lakini kocha kijana wa Simba anayekubalika zaidi na mashabiki, Masoud Djuma amewaambia kwamba majibu yatapatikana uwanjani huku wakimpa majukumu Shiza Kichuya.

Mtibwa yenye pointi 30, inawakaribisha Simba kesho Jumatatu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro ikiwa imeshinda michezo yake miwili mfululizo ule wa FA dhidi ya Azam FC na wa ligi baina ya Singida United timu ambazo zote zinaongozwa na makocha wa kigeni huku wao wakiongozwa na mzawa Zuber Katwila.

Kichuya apewa majukumu Straika mwenye mizuka ndani ya Simba, Shiza Kichuya amekabidhiwa majukumu mazito na kocha mkuu wa timu hiyo, Mfaransa, Pierre Lechantre kuhakikisha anaimaliza Mtibwa.

No comments