Header Ads

KOCHA WA BARCELONA AMESEMA HANA MPANGO WA KUMSHAWISHI INIESTA

Nikufahamishe kuwa kocha wa Barcelona, Ernest Valverde amesema hana mpango wa kumshinikiza Andres Iniesta kubakia katika timu ya Barcelona. Iniesta amewahi kukaririwa siku za nyuma akisema kuwa atafanya uamuzi mwishoni mwa msimu huu ikiwa kama atabakia katika timu hiyo au ataondoka.

Kiungo huyo amekuwa na Barcelona tangu mwaka 1996, ambako alijiunga na timu ya watoto na alianza kuchezea timu ya wakubwa 2001.

Andres Iniesta anadai kuwa amepokea ofa nyingi zikiwamo za kwenda kucheza soka ya kulipwa nchini China.

Kocha Valverde alisema hahitaji kumshinikiza au kumshawishi abaki kwa kuwa yeye mwenyewe (Iniesta) anajua anavyokubalika ndani ya klabu ya Barcelona.

No comments