Header Ads

KOCHA WA JUVENTUS AMLINGANISHA RONALDO NA MVINYO

Massimiliano Allegri kocha wa timu ya Juventus amemfananisha mchezaji Cristiano Ronaldo na kinywaji cha mvinyo akisema kuwa kadiri umri unavyokwenda ndio anazidi kuwa mkali zaidi.
Kocha huyo Allegri alimkubali Ronaldo baada ya kuiongoza Real Madrid kuirarua Juventus kwa mabao 3-0 mbele ya mashabiki  kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, wiki iliyopita.
Ikumbukwe  Ronaldo aliacha mashabiki wa soka mdomo wazi baada ya kufungia timu yake ya Real Madrid bao maridadi la ‘tik tak’.

Allegri aliongezea  kuwa kiungo huyo amekuwa straika bora wa dunia kwa miaka miwili sasa.

Alisema kuwa pamoja na fowadi huyo kuwa na umri wa miaka 33 lakini bado ana kiwango cha kutisha.

Katika miaka ya nyuma, Ronaldo alikuwa anasifika kwa mbio na chenga lakini kutokana na umri kumtupa mkono siku hizi anahakikisha anakuwa kwenye nafasi nzuri ya kufunga kila mara.

No comments