Header Ads

MBOWE NA VIONGOZI WENGINE WA CHADEMA WALIVYOINGIA MAHAKAMANI LEO

Leo April 13, 2018 mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe na Viongozi wenzake watano tayari wameshafikishwa mahakama ya kisutu ni tangu saa mbili asubuhi hii na sasa wanasubiri shughuli za kimahakama zianze ili wakamilishe masharti ya dhamana.

Mbali ya Mbowe wengine ni Katibu Mkuu Dk Vicent Mashinji, Manaibu Katibu wakuu John Mnyika (Bara), Salum Mwalimu (Zanzibar), Mbunge wa Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa na Mweka Hazina wa Baraza la Wanawake wa chama hicho Ester Matiku wanakabiliwa na kesi ya jinai, wakidaiwa pamoja na mambo mengine ikiwamo kufanya mikusanyiko na maandamano yasiyo halali.

Wamekuwa mahabusu tangu walipopandishwa kizimbani na kusomewa mashtaka hayo March 27, 2018.

No comments