Header Ads

HALIMA MDEE ASOMEWA MASHTAKA , VIONGOZI WA CHADEMA WATIMIZA MASHARTI YAO

Mbunge wa Kawe, Halima Mdee  yeye amesomewa mashtaka mawili ya kufanya mkusanyiko usio halali na kuendelea na mkusanyiko huo, kutotii amri iliyowataka kutawanyika na kusababisha vurugu iliyosababisha kifo cha Akwilina Akwilini na askari kujeruhiwa. 

Kwa upande wa viongozi 6  wa Chadema wakiongozwa na Mwenyekiti wao Freeman Mbowe wametimiza masharti ya dhamana Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Washtakiwa hao walitakiwa kila mmoja kuwa na wadhamini wawili ambao watasaini hati ya dhamana ya Sh20 milioni na kuwa na barua kutoka kwa viongozi wao ama wa vijiji au mtaa, ambao watapaswa kuwa na nakala za vitambulisho vyao.

No comments