Header Ads

HUYU NDIYE WINNIE MADIKIZELA MANDELA

Winnie Madikizela-Mandela ni miongoni mwa wanawake shupavu ambao wamewahi kutokea kwa kuwa mstari wa mbele katika kupambana na vita dhidi ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.
                      Winnie Madikizela-Mandela
Mke huyo wa rais wa zamani Hayati Nelson Mandela, amefariki Jumtatu hii akiwa na umri wa miaka 81 kutokana na kuugua kwa muda mrefu. Hapa chini fahamu japo kwa ufupi maisha ya mama huyo ambaye atakumbukwa kwa kukumbukwa muda wote.
Winnie Mandela alizaliwa 26 September, 1936 katika eneo la Mbizana. Aliwahi kuwa Dada Mkuu katika shule ya Bizana na alisomea kazi ya utoaji huduma za kijamii katika shule ya Jan Hofmeyr School na haraka aliyazoea maisha ya kuwa mama na mwanasiasa.

Wawili hao walitengana mwaka 1992 na March 1996 Mandela alimpatia talaka Winnie. Hata hivyo mwaka 1994 Winnie alipoulizwa kuhusu kupatanishwa na mumewe Mandela alisema: “I am not fighting to be the country’s First Lady. In fact, I am not the sort of person to carry beautiful flowers and be an ornament to everyone.”
Wakati ambao Mandela alifungwa gerezani mwaka 1964 bila ya kuwepo kwa matumaini ya kuachiwa huru kutokana na hukumu ya kifungo cha maisha jela alichopewa, Winnie alilazimika kubeba jukumu la kulea mwenyewe wa watoto wao na kuendeleza kampeni za kisiasa zilizolenga kutaka mashujaa wa kupigania nchi yao waachiwe huru akiwemo mumewe.

Mwaka 1969 mama huyo alifungwa kifungo cha miezi 18 jela katika gereza la Pretoria Central Prison na hata kuwekwa katika kizuizi cha pekee yake ambacho ni mojawapo ya vifungo vigumu zaidi gerezani vinavyowaathiri wafungwa wengi saikolojia.
Pia amekuwa muungaji mkono mkubwa wa kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighters cha Julius Malema , kilichojimegua kutoka ANC ambacho kilimkosoa vikali rais aliyelazimika kung’atuka Jacob Zuma.

No comments