Header Ads

APANDISHWA CHEO BAADA YA KUELEZA UKWELI MBELE YA RAIS MAGUFULI

Rais Dkt. John Magufuli amemuagiza Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango kumpandisha cheo Kaimu Kamishna wa Forodha na Ushuru wa Bidhaa wa TRA bandari ya Dar es Salaam Ben Usaje na kuwa Kamishna kamili bandarini hapo ndani ya wiki hii.

Dkt. Magufuli ametoa agizo hilo wakati alipokuwa anazungumza na  viongozi mbalimbali kwenye bandari ya Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake ya kushtukiza kwenye bandari na kusema amefanya hivyo kutokana na kazi nzuri aliyoifanya Ben Usaje katika kusimamia maslahi ya nchi vizuri.

No comments