Header Ads

VIDEO:KIFO CHA MZEE MAJUTO,Mwili wake Kuagwa Karimjee Leo



Mwili wa msanii wa vichekesho Amri Athumani ' King Majuto' aliyefariki jana katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, utaagwa leo Agosti 9, 2018 katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

Rais wa shirikisho la filamu Tanzania , Simon Mwakifamba amesema, Mzee Majuto ataagwa kuanzia saa 8.00 mchana katika viwanja hivyo na saa 10.00 jioni atasafirishwa kwenda nyumbani kwake Tanga kwa mazishi.

“Taarifa ambayo tumewasiliana na familia ni kwamba, Mzee Majuto ndugu jamaa na marafiki watatoa heshima za mwisho na baada ya hapo mwili utaelpelekwa nyumbani kwake Tanga kwa ajili ya mazishi,” amesema Simon Mwakifamba

Kwa upande mtoto wa Mzee Majuto, Ashrafu amesema,ratiba kamili ya mwili wa Mzee Majuto ni kwamba asubuhi  mwili utaandaliwa katika Hospitali ya  Muhimbili na shughuli zote ndogo ndogo zitafanyika hapo, baada ya hapo mwili utapelekwa Karimjee kwa ajili ya kuagwa saa nane mchana," anasema

No comments