Aguero afunga 'hat-trick' na kuisadia Man City kuicharaza Watford 6-0
Sergio Aguero alifunga hat-trick na kuisadia Manchester City kupanda katika kilele cha jedwali la ligi baada ya kuwashona Watford mabao sita bila jibu.
Watford ambao walikuwa hawajafungwa wangepanda hadi katika kilele cha jedwali la ligi iwapo wangepata ushindi dhidi ya kikosi cha Guardiola, lakini walishangazwa na safu ya mashambulizi ya City ambayo imefunga mabao 15 katika mechi tatu.
Aguero alianza kwa kufunga mpira wa adhabu uliopigwa na Kevin De Bruyne kabla ya kuugusa mpira karibu na goli na kupata bao la pili baada ya dakika nne na hivyobasi kufanya mambo kuwa 2-0 kufuatia pasi nzuri kutoka kwa David Silva.
Gabriel Jesus aliongeza bao la tatu likiwa ni lake la tano msimu huu baada ya kufunga bao zuri kutokana na pasi iliopigwa na Aguerro.
Na licha ya madai kwamba alikuwa ameotea kutoka kwa mabeki refa aliotesha mpira kupelekwa katikati ya uwanja.
Watford ilikuwa imecheza mechi tatu bila kufungwa msimu huu na ilionekana imeimarika baada ya kipindi cha kwanza ,huku Andre Carillo na Richarlison, wote wakipata nafasi nzuri ya kushambulia.
Lakini City iliendelea kusonga mbele na kuongeza mabao mengine matatu.
Nicolas Otamendi alifunga kwa kutumia kichwa kutokana na kona iliopigwa na David Silva kabla ya Aguero kufunga bao lake la tatu, baada ya kuvamia ngome ya Watford akiwa pekee ndani ya eneo hatari.
Raheem Sterling alifunga bao la sita kupitia mkwaju wa penalti baada ya kuangushwa na Christian Kabasele.
Matokeo mengine:
No comments