Chelsea kukabiliana na Arsenal darajani
Eden Hazard amepona jeraha la kifundo cha mguu na anaweza kuanza mechi yake ya kwanza tangu msimu uanze dhidi ya Arsenal.
Nahodha Gary Cahil huenda akarudi katika kikosi cha kwanza baada ya kuonyesha mchezo mzuri katikati ya wiki, lakini kiungo wa kati Drink Water anauguza jeraha la nyonga na hatocheza hadi mwezi ujao.
Mshambuliaji wa Arsenal Theo Walcot huenda asishiriki katika mechi hiyo baada ya kupata jeraha la nyonga katika ligi ya Yuropa.
Kiungo wa kati Francis Coquelin hatocheza kutokana na jeraha la goti huku Santi Carzola akiendelea kukaa nje.
No comments