Header Ads

CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WANAFUNZI KATIKA VYUO VYA NDANI NA VYA KIGENI

Na PASCHAL D.LUCAS,


MUHULA  wa kwanza wa masomo pindi unapokuwa chuo hasa kwa wanafunzi wa kimataifa huwa ni vigumu kuweza kukabiliana na mazingira ya chuo na nchi husika kwa ujumla.
Hizi ni baadhi ya changamoto ambazo huwakumba wanafunzi wa kigeni pindi wanapokwenda kujiunga na vyuo vya kimataifa.




Majaribio mapya
Mbali na kukabiliwa na hali mpya ya hewa lakini pia eneo hili ni moja ya changamoto ambayo huwasumbua wanafunzi wa kigeni kwenye vyuo vya kimataifa wanapoingia kwa mara ya kwanza, kwanza mwanfunzi anakuwa hajapata matirio ya kutosha lakini pia anakuwa hajafahamu aina ya majaribio ambayo yamekuwa yakitolewa na mwalimu husika.
Mbali na hilo pia jaribio hili huchukuliwa na mkufunzi kama kipimo cha nani ni nani darasani na hivyo kujikuta wengi wakihofia juu ya kufanya vizuri jambo litakalowafanya waaminiwe na walimu husika.
Walimu
Hili liko wazi kuwa unapojiunga na maasomo ya chuo hasa vyuo hivi vya kimataifa lazima utakutana na wakufunzi wapya ambao ni wageni kwako kwa maana ya maprofesa, mfano kwa nchi kama Marekani wakufunzi wengi hupendelea kuona wanafunzi wakijumuika na kushirikiana pamoja kwenye eneo la masomo.
Lakini kwa wanafunzi wa kigeni huwa ni ngumu zaidi kupata ushirikiano wa haraka kwa wakufunzi hao hivyo hulazimaka kuanza kutengeneza mazoea kwa kufanya vizuri darasasani.
Masomo
Vyuo vingi huwaomba wanafunzi kuchukua seti nzima ya masomo ya fani wanayotaka kusoma ambapo kwa namna nyingine kuna baadhi ya masomo ambayo yanakuwa ni mapya kwao hivyo kujikuta wakianza moja.
Utaratibu huu umekuwa ukiwashangaza zaidi wanafunzi wanaoenda kusoma kwenye vyuo vya nje ambao hufika kwenye vyuo hivyo kwa lengo moja la kusoma kama ni biashara au uhandisi pekee bila kuhusisha mambo mengine.
Marafiki
Maisha ya chuo hayaishii darasani pekee  kwani wanafunzi wengi hupenda kujifunza mambo ambayo huwa yanaendelea nje ya masomo ili kufahamu utamaduni wa taifa husika na mambo muhimu.
Wanafunzi wengi wa kimataifa husema kuwa ni jambo la busara kujichanganya na watu uliowakuta kwa ajili ya kujifunza mambo mapya na kujenga urafiki, kujifunza tamaduni na kujifunza masuala mengi yanayohusiana na elimu kwa ujumla.
Moja ya maeneo ambayo wanafunzi wengi wa kigeni hukutana na marafiki ni klabu za usomaji, majadiliano na matukio mbalimbali.
Chakula
Kwenye mataifa kama Marekani kuna vyakula vya aina tofauti ambavyo kwa wanafunzi wa kigeni huwachukua muda kidogo kuvizoea na hivyo kujikuta kwa siku za mwanzoni wakila vyakula ambavyo ni rahisi na haviwezi kuwaletea madhara.
Kwani wanafunzi wa kigeni kupokea ubora wa chakula husika huwa ni changamoto kubwa ambayo hutokana na mazoea ya mwanafunzi alikotokea kwani wakati mwingine vyakula alivyozoea kula nyumbani vinakuwa ni ngumu kupatikana kwenye nchi anayosoma.
Mfano mlezi wa wanafunzi katika chuo kikuu cha Drake cha Marekani anasema kwa wiki ya kwanza ambayo wanafunzi hufika chuoni hapo wengi hupendelea kula pizza, kuku, wali na baadhi ya nyama kutokana na kushindwa kuzoea kula vyakula vingine kama samaki vinavyopatikana huko.
Kuwaza nyumbani
Hii pia ni moja ya sababu ambayo huwakabili wanafunzi kwani wengi huwachukua muda mwingi mawazo ya kule walikotoka kuondoka na hivyo kujikuta wakiwa wanyonge.
Utamaduni
Changamoto nyingine ambayo ni kubwa ni ila ya utamaduni kwani wanafunzi wengi huja na tamaduni zao walizozizoea na hivyo kujikuta wakilazimika kujifunza utamaduni mpya kulingana na taifa husika licha ya kuwa jambo hili linatazamwa kama changamoto lakini lina faida pia kwa wanafunzi wenyewe.
LughaHii nayo imekuwa ni moja ya sababu kubwa ndiyo maana wanafunzi wengi wamekuwa wakisisitiziwa kujifunza lugha mbalimbali jambo ambalo litamrahishia kupata huduma kirahisi hata kwenye vyuo vya kigeni.
Kama wewe ni mwanafunzi haijalishi kwamba unakumbana na changamoto gani jambo la msingi ni kutambua kuwa hauko peke yako mgeni, hivyo siri ni kushirikiana na wenzako ambao utaona mnaelewana na hapo ndipo unaweza kuwa mwanzo wa wewe kuanza kufurahia maisha mapya ya chuo.

No comments