Marekani yajadili kufunga ubalozi wake Cuba
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema Washington inajadili iwapo ifunge ubalozi wake nchini Cuba, baada ya kutokea mlolongo wa mashambulizi ya kelele kwa wafanyakazi wake.
Zaidi ya wafanyakazi 20 wa ubalozi wa Marekani wameripotiwa kuwa na matatizo ya afya ya ubongo na wengine wakipoteza uwezo wa kusikia kutokana na mashambulizi hayo.
Marekani imeiambia Havana kwamba jukumu la kuwalinda wafanyakazi wake na nchi nyingine lipo juu yao.
Uchunguzi zaidi unaendelea kujua chnzo cha watu hao kutosikia.
No comments