Marekani na mabadiliko ya tabia ya nchi
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Marekani Rex Tillerson ameonyesha ishara ya jinsi Ikulu ya ncjhi hiyo ilivyo na nia ya kujihusisha tena na makubaliano ya kimataifa kupambana na mabadiliko ya tabia ya nchi, licha ya Rais wa nchi hiyo Dobald Trump kutangaza kwamba ataitoa nchi hiyo nje ya mkataba wa Paris.
Rex Tillerson ameshauri kuwa Marekani inaweza kujadili tena mkataba huo kwa masharti yenye kufaa zaidi.
Katika mahojiano tofauti ya Interview, Mshauri wa Masuala ya Usalama wa Taifa wa Marekani H.R McMaster amesema Rais Trump yuko wazi kwa mazungumzo yoyote ambayo yataimarisha mazingira.
No comments