Header Ads

Hakuna tena Mgogoro wa Kibiashara Tanzania na Kenya





Nchi za Tanzania na Kenya zimetimiza agizo la maraisi wake na kukubaliana kuondoa vikwazo vya biashara katika bidhaa za unga wa ngano na gesi ya kupikia kutoka Kenya na zile za Maziwa na Sigara kutoka Tanzania.

Aidha masuala mengine 15 kutoka Tanzania na 16 ya Kenya bado yako mezani na majadiliano yanaendelea.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, wakati wa kuhitimisha mazungumzo ya kibishara baina ya nchi hizo ya Siku mbili, Katibu Mkuu wa biashara na uwekezaji nchini Tanzania Adolph Mkenda amesema wamefikia makubaliano hayo ya kibiashara ili kuhakikisha wanatimiza matakwa ya viongozi  wakuu, Rais John Pombe Magufuli na Uhuru Kenyata, yaliyoyowataka wafanye kazi na kuondoa vikwazo vya  biashara mara moja katika nchi hizoi mbili kubwa ndani ya jimuiya ya Africa Mashariki,

Amesema, baada ya maagizo yao, kwa kushirikia na Katibu Mkuu wa biashara wa Kenya, Dr Chris Kiptoo walianza kuwasiliana kwa karibu ambapo kwa kuanzia walifanya mkutano katika mpaka wa Namanga kuangalia biashara inavyokwenda na vikwazo vilivyopo katika nchi hizo ambavyo vilitatuliwa baada ya kupitia masuala mbali mbali,

 Aidha amesema kupitia majadiliano hayo, wameweza kupatia ufumbuzi mambo mengi ikiwemo biashara ya ngano, ambapo amesema wamekubaliana kifungua biashara ya ngano katika nchi hizi na kuhahakikisha wanaiboresha zaidi ikiwamo kutoa kipaumbele kwa wakulima wa zao hilo.

"Tulipata fursa ya kukaa na wadau wa biashara ya unga na ngano yenyewe kutoka nchi hizi mbili, wakiwemo wadau wenye viwanda vya kusaga ngano, wakulima na maafisa wa wizara za kilimo kutoka nchi zote ambao tumekubakiana kufungua biashara ya unga wa ngano kati ya Kenya na Tanzania, na sasa hivi unga wa ngano unapita unavuka mpaka bila vikwazo vyovyote." Amesema Mkenda

Kenya sasa hivi inazalisha ngano nyingi kuliko Tanzania na Tanzania ina uwezo mkubwa wa kuzalisha ngano kuliko Kenya hivyo tukiunganisha biashara na uwezeshaji,ngano ya Kenya itaongezeka na maeneo mengi Tanzania ambayo yanauwezo wa kuzalisha ngano yataongeza uzalishaji wa ngano

Aidha alisema wamekubaliana na wenye viwanda waanze kutumia ngano za kutoka nchini kabla kuagiza kutoka nje ya nchi hizi mbili na waonyeshe nia nzuri ya kujenga ushirikiano Wa jumuiya hii ya Africa Mashariki..

Kwa upande wake, katibu Mkuu Wa Kenya, Dr Chris's Kaptoo amesema, Kenya imewekeza zaidi dola bilioni moja na nusu nchini Tanzania kwa ajili ya masuala mbali mbali ya kibiashara na viwanda ambapo watu zaidi ya elfu 50 wameajiriwa.

 Ameogeza katika kuendeleza biashara katika nchi hizi mbili, watatumia Uchumi na Nakumati supermarket na kuhakikisha zinafanya kazi inavyopaswa na wale wanaopeleka bidhaa zao wanalipwa kwa wakati.
"Tunafanya bidii kuona Uchumi Supermarket inaimarika, tunataka matawi yake yote yaliyokuwepo Tanzania yanaendelea kama yalivyokuwa awali na pia wale wote watakao kuwa wanapeleka bidhaa zao huko wanalipwa kwa wakati" amesema Dr Kiptoo"

Amesema, siyo wajibu wake yeye katibu kuingilia biashara za watu binafsi kama Nakumat na Uchumi lakini kwa umuhimu wa biashara wanaingilia kati kuhakikisha iko salama na inatimiza matakwa ya nchi.

No comments