Header Ads

Kimbunga Maria chaleta hofu, caribbean

Kimbunga MariaHaki miliki ya pichaNASA
Image captionKimbunga Maria
Marekani imesema kimbunga Maria kinatarajia kupiga katika visiwa vya Leeward vilivyoko mashariki mwa Caribbean.
Kituo cha Marekani kinachioshughulika na vimbunga kimesema kimbunga hicho pia kinatarajiwa kupita karibu na Dominica katika saa chache zijazo.
kikiwa katika eneo hilo kimbunga hicho kinatarajiwa kuleta madhara makubwa.
Kimbunga Maria kwa sasa upepo wake umekuwa ukifululiza kwa kilomita mia mbili hamsini kwa saa.
Kituo cha Marekani kinachoshughulika na vimbunga kimesema visiwa vya Dominica, Guadeloupe na Martinique vinatarajiwa pia kupitiwa na kimbunga hicho na uwezekano wa kutokea kwa dhoruba kali.
Wakaazi wa kisiwa cha Martinique wametakiwa kubaki ndani.
Kimbunga Maria kimekuwa kikitishia visiwa vingi ambavyo vimekumbwa na madhara makubwa ya kimbunga Irma mapema mwezi huu.

No comments