Israel na Marekani zaanzisha kambi ya pamoja ya jeshi la anga
Israel na Marekani zimeanzisha kambi ya pamoja ya jeshi kwa mara ya kwanza katika historia.
Mkuu wa jeshi la anga la Israel Brigedia Jenerali Tzivka Heimowitz amesema kuanzishwa kwa kambi hiyo ya pamoja ambayo haijawekwa wazi eneo ilipo, sio kwa nia ya kufanya vitisho kwa nchi yeyote.
Tukio hilo limefanyika muda mfupi kabla ya Rais Trump kukutana na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu katika kikao cha umoja wa mataifa mjini New York.
No comments