Header Ads

TAKUKURU Lindi yawatangazia ubaya waliojinufaisha na waliovuruga ugawaji wa pembejeo kwa wakulima wa korosho

Ahmad Mmow,Lindi.
KAMA ULIDHANI waliojinufaisha na waliovuruga zoezi la ugawaji pembejeo  zilizotolewa na serikali kwa wakulima wa korosho mkoani humu  wataendelea kudunda mitaani bila kushugulikiwa utakuwa unajidanganya.

Taarifa zisizo na chembe ya shaka kutoka kwa vyanzo makini na vyakuaminika ndani ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU),mkoani humu zimeeleza kuwa taasisi hiyo imeanza uchunguzi kwa kasi ya kutisha.

Vyanzo hivyo ambavyo vilikataa katakata kutajwa majina yake kwenye habari hii kwa madai kwamba havinamamlaka kisheria kuzungumzia mambo hayo(Siowasemaji) vimeeleza na kuapa hakuna jiwe litakalo salia baada ya uchunguzi huo kukamilika.

"Viongozi wakuu wa nchi wameagiza,unadhani ninani atapuuza.Uchunguzi umeanza tangu kitambo,unakwenda vizuri nakwakweli kunawatu wamevuruga na wamejinufaisha,sisi tutawasomba wote walivuruga na walionufaika na uvurugaji huo kuanzia wakubwa hadi wadogo,"alisema mmoja wa maofisa wa taasisi hiyo kutoka kitengo cha uchunguzi.

Ofisa huyo alisema kunaukweli kwamba wapo watu ambao hawana mashamba na majina yao hayapo kwenye orodha iliyopitishwa na mikutano mikuu ya vijiji lakini yanaonekana kwa baadhi ya wataalam wa idara zenye thamana ya kilimo na mifugo na wamepata pembejeo.

"Lakini pia wapo waliopewa dawa na viwatilifu vingi tofauti na idadi ya  mikorosho waliyonayo. Wakati wakulima wengine wamegwana mfuko mmoja wa salfa watu wanne, mtu mwingine amepata mifuko 40 akiwa na mikorosho 20, na mwingine hana kabisa.Wote hao tutawaburuzia mahakamani,"alisisitiza ofisa huyo.

Maelezo ya ofisa huyo yaliungwa mkono na Ofisa mwingine aliyesema licha ya kuendelea na uchunguzi lakini pia taasisi hiyo imeanza kuwadaka baadhi ya wanufaika wa uvurugwaji wa zoezi la ugawaji.

Alisema lengo nikupata na kukamata mnyororo mzima uliovuruga na kujinufaisha kuanzia  juu hadi chini kabisa.Ambapo kwa wanufaika wadogo ambao baadhi yao hawana mashamba nirahisi kuwapata na ndio walioanza kukamatwa.Bali umakini mkubwa wa uchunguzi upo kwa waliovuruga.

" Huko ndiko tunakochambua nyaraka na kuoanisha.Tumeanza kubaini madudu kadhaa,zoezi linakewnda vizuri hakuna atakae salimika wewe utasikia na utaona pia,"aliapa ofisa huyo aliyeonekana yupo kwa muda mrefu serikalini.

Kwakuwa maofisa hao walisema sio wasemaji wa taasisi hiyo,Muungwana ililazimika kumpata mwenye haki ya kusema,ambae ni kamanda wa TAKUKURU wa mkoa wa Lindi,Steven Chami.

Kamanda Chami ambae hakutaka kuingia kwa undani kuzungumzia jambo hilo licha ya kukiri kuwa uchunguzi kuhusu hayo  unafanyika,alisema uchunguzi unaondelea sio wa pembejeo zilizotolewa na serikali zigawiwe bure kwa wakulima katika msimu wa 2017/2018 tu,bali hata misimu iliyopita.

"Siwezi kueleza tumefikia hatua gani nawahusika wakuu ninani,bali uchunguzi unaendelea.Tena tunachunguza hata madudu ya misimu ya nyuma,muda ukifika mtajulishwa rasimi,"alisema kwa umakini na tahadhari kamanda Chami.

Akifunga maonesho ya wakulima kitaifa ya mwaka huu katika viwanja vya Ngongo Manispaa ya Lindi.Makamo wa Rais ,Samia Suluhu Hassan alimtaka waziri wa kilimo,uvuvi na mifugo kuwashugulikia watendaji wa serikali waliohujumu na kuvuruga zoezi la ugawaji wa pembejeo kwa wakulima wa korosho mkoani humu na maeneo mengine yanayolima zao hilo.

No comments