Kuwait yamfukuza balozi wa Korea Kaskazini
Ripoti kutoka nchini Kuwait zinasema kuwa imemfukuza balozi wa Korea Kaskazini.
Hakuna taarifa rasmi iliyotolewa lakini kuwait imewaambia waandishi wa habari kuwa balozi wa Korea Kaskazini, amepewa mwezi mmoja kuondoka huku wanadiplomaisa wa Korea Kaskazini wakipunguzwa.
Kuwait ndiyo nchi pekee katika ghuba iliyo na ubalozi wa Korea Kaskazini.
- Mzozo wa Qatar na jirani zake
- Bei ya mafuta: Amir wa Kuwait avunja bunge
- Njiwa ashikwa na mfuko 'uliojaa mihadarati'
- Serikali yamnyonga mwanamfalme Kuwait
Maelfu ya raia wa Korea Kaskazini wanafanya kazi nchini kuwait na nchi zingine za ghuba kama vibarua.
Hatua hiyo inachukuliwa wiki mbili baada ya kiongozi wa kuwait kuzuru Washington.
Marekani imetaka hatua za kimataifa kuchukuliwa dhidi ya Korea Kaskazini kufuatia mipango yake ya nyuklia.
No comments