Header Ads

Maandamano baada ya polisi mzungu kuondolewa mashtaka ya kumuua mtu mweusi Marekani

Protesters march through the West County Center in St Louis' Des Peres suburb. Photo: 16 September 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaandamano baada ya polisi mzungu kuondolewa mashtaka ya kumuua mtu mweusi
Maandamano mapya yametokea katika mji wa St Louis nchini Marekani, ambapo polisi mzungu wa zamani alipatwa kutokuwa na hatia kwa kumuua mtu mweusi mwaka 2011.
Mamia ya watu waliandaanama katika mji wa Missouri kwa siku ya pili wakisema kuwa maisha ya weusi yana maana.
Zaidi ya waandamanaji 33 walikamatwa na polisi 11 kujeruhiwa wakati wa ghasia za siku ya Ijumaa usiku.
Polisi huyo Jason Stockley 36, aliondolewa mashtaka ya kumuua Antony Lamar Smitjh 24.
Jumamosi jioni, polis walitokea wakati waandamanaji walikusanyika katika mji wa St Louis.
Protesters clash with police in St Louis. Photo: 15 September 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMaandamano baada ya polisi mzungu kuondolewa mashtaka ya kumuua mtu mweusi
Umati ulitembea katika barabara za Des Peres na kufunga barabra moja kuu.
Bwana Smith alikuwa baba na alikuwa afunge ndoa wakati aliuawa tarehe 20 Desemba mwaka 2011.
Bwana Stockley na mwenzake walisema waliamini kuwa Bw Smith alikuwa akishriki katika kitendo kinachohusu madawa ya kulevya nje ya mkahawa.
Lamar SmithHaki miliki ya pichaCBS
Image captionBwana Smith alikuwa baba na alikuwa afunge ndoa wakati aliuawa tarehe 20 Desemba mwaka 2011.
Video ya polisi ilionyesha Bw Smith akirudisha gari nyuma kwenda kwa lile la polisi mara mbili katika jaribio la kutoroka.
Baada ya kumfuata kwa kasi kwa muda wa dakika tatu, Bw Stockley alimuambia mwenzake ambaye alikuwa akiendesha gari aligonge gari la Smith.
Bwa Stockley kisha akakimbia kwenda kwa dirisha la gari la Smith na kumfytulia risasi mara tano.
Jason StockleyHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionPolisi Jason Stockley


No comments