Umri mzuri kwa mwanamke kupata mtoto (kuzaa)
Na Paschal D.Lucas
Tamaa ya kutaka kufanikiwa maishani imeenea duniani kote. Hali imebadilika sana, jinsia ya kike inataka kujitosheleza kwa kila kitu. Lakini mabadiliko ya kibaiolojia yanabaki vile vile mfano kuzeeka nk.
Mafanikio wanayowaza wengi ni utajiri wa pesa na elimu kubwa. Hii imesababisha wanawake wengi kusoma sana na kufanya kazi kupita kiasi, hata kupuuzia suala la kuzaa mapema.
Watu wengi wanashtuka wakiona umri wao unafikia au kuwa zaidi ya miaka 30, ndio wanakuwa na tamaa ya kuzaa. Kuchelewa kwao kuzaa kunaweza kuwa kwa taabu ama kuzaa watoto wenye matatizo mengi ya kiafya.
Kwa miaka mingi, wataalamu wengi wa afya ya uzazi bado wanaamini miaka 20-35 ndio umri sahihi kushika mimba na kuzaa.
Utafiti uliochapishwa kwenye jarida la magonjwa ya uzazi (Journal of Obstetrics & Gynacology) uliofanywa na watafiti kutoka Taasisi ya Karolinska ya nchini Sweden umegundua katika nchi tajiri duniani wanawake huzaa wakiwa na umri mkubwa kitu kinachopelekea kuongezeka kwa hatari ya kuzaa watoto njiti (Preterm birth), ukuaji hafifu wa vichanga na kuzaa watoto wafu (Stillbirth).
Ijapokuwa, wengi hufikiri matatizo mengi ya uzazi huongezeka baada ya miaka 35 na huwa zaidi baada ya miaka 40.
Kwa wenzi wawili wanaoishi pamoja, kuchelewa kuzaa huathiri pia wenza wa kiume, ambapo mbegu za uzazi za mwanaume hudhorota kila mwaka upitao na watoto wamaotokana na wanaume wazee huwa na hatari zaidi ya kupata matatizo ya akili na matatizo ya chembe za urithi.
No comments