Wanaume washindwa kuzalisha kwa sababu ya Mirungi Same
Same.Imeelezwa kwamba idadi kubwa ya wanaume hawana uwezo wa kuzaa kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya kwa muda mrefu ikiwemo mirungi na bangi.
Kutokana na hali hiyo Mbunge wa Same Mashariki Naghenjwa Kaboyoka, amemwomba Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kuingilia kati ili kuokoa vijana.
Kaboyoka amesema wananchi wengi wanajishughulisha na ulimaji wa zao hilo bila kuogopa sheria hususan za mamba vunta na Gonja.
Amesema sababu ya ulimaji na utumiaji wa bangi na mirungi ni kutokuwepo kwa kituo cha polisi katika maeneo hayo.
Amesema ameshaongea na Waziri Nchemba ambaye na amemuahidi kujenga kituo cha polisi katika maeneo hayo
ili kupunguza ulimaji wa mirungi na bangi lakini ni mwaka sasa umeshapita.
“Nikiwa katika bunge la mwisho niliongea na Katibu Mkuu wa Mambo ya Ndani kwamba ulimaji wa mirungi, bangi pamoja na uhalifu ni mkubwa na unazidi kushika kasi katika tarafa hizo."amesema Kaboyoka
Kaboyoka amesema usafiri wa kwenda kuripoti matukio ya kihalifu ni changamoto ya usafiri ambapo basi linatoka saa nane usiku hadi kurudi kesho yake.
“Sasa fikiria wahalifu watapelekwaje ,na nani atenda kuripoti na basi linaloondoka sa nane, hivyo uhalifu unazidi kuongezeka kutoka na kwamba hakuna wakuwakamata”amesema Kaboyoka.
Naye Katibu Tawala wa Wilaya hiyo,Sospeter Magonera amesema wanapinga vikali kilimo hicho cha mirungi kutokana na kwamba kipo kinyume na sheria za nchi.
“Kilimo hicho kinachangia kwa asilimia kubwa kuharibu nguvu kazi ya jamii pamoja na nguvu kazi ya Taifa hali ambayo inarudisha maendeleo ya taifa nyuma”amesema Sospeter
Hata hivyo,diwani wa kata ya mamba miamba, Michael Mauya amesema uvutaji wa bangi na utumiaji wa mirungi umechangia kwa asilimia kubwa vijana kuishiwa nguvu za kiume hali ambayo imechangia kupungua kwa idadi ya watoto katika tarafa hizo.
No comments