Bodaboda yapigwa stop Zanzibar
Serikali imesema haijatoa lesseni za usafiri wa pikipiki (bodaboda) kusafirisha abiria kwa njia ya biashara na atakae tumia bodaboda kusafirisha abiria atakuwa ametenda kosa kisheria hivyo hatua kali zitachukuliwa.
Naibu Waziri wa Ujenzi,Mawasiliano na Usafirishaji Mohammed Ahmda Salum amesema licha ya kuwa serikali haina ajira za kutosha lakini ajira ya bodaboda bado haijaruhusu kufanyika Zanzibar kutokana na athari nyingi zinazotokea zinazotokana na bodaboda hizo.
Amesema Serikali inawashauri vijana kufanya ajira halali zilizoruhusiwa kisheria ili kuepusha mizozo na serikali na kutoa wito kwa waendesha pikipiki kuwa makini na kufuata sheria wanapokuwa barabarani ikiwemo kuvaa kofia ngumu ambayo itamkinga endapo watapata ajali.
No comments