WATU 30 WAUWAWA SOMALIA
Mji wa Mogadishu umekuwa ukilengwa na kundi la wapiganaji wa al-Shabab ambalo linakabiliana na serikali.
Shambulio la bomu kubwa katika eneo lenye watu wengi katika mji mkuu wa Mogadishu nchini Somalia limewaua takriban watu 30, kwa mujibu wa polisi.
Makumi wengine walijeruhiwa wakati lori lililoegeshwa na vilipuzi kulipuliwa karibu na lango kuu la hoteli.
Polisi wanasema kuwa watu wawili waliuawa katika mlipuko mwengine wa pili katika wilaya ya Madina iliopo katika mji mkuu.
Haijulikani ni nani aliyetekeleza shambulio hilo.
Mji wa Mogadishu umekuwa ukilengwa na kundi la wapiganaji wa al-Shabab ambalo linakabiliana na serikali.
- Watu 15 wauawa kwa bomu Somalia
- Mlipuko mkubwa wakumba eneo la bandari ya Mogadishu Somalia
- Shambulizi la bomu laua watu 10 Mogadishu
Baada ya mlipuko wa kwanza, afisa mkuu wa polisi Mohammed Hussein aliambia chombo cha habari cha Reuters :lilikuwa bomu lililotegwa katika lori.
''Kuna majeraha mengi lakini hatujui idadi yao kwa kuwa eneo hilo bado linachomeka''.
Mashahidi waliambia BBC wanaamini makumi ya watu wamefariki.
Ripota wa BBC nchini Somalia katika eneo hilo alisema kuwa hoteli ya Safari ilianguka huku watu kadhaa wakidaiwa kukwama chini ya vifusi vyake.
Mkaazi wa Mogadishu Muhidin Ali aliambia chombo cha habari cha AFP: Kulikuwa mlipuko mkubwa kuwahi kutokea , uliharibu eneo lote
No comments