Header Ads

MVUA YASABABISHA WAKAZI WA MTWARA KUKOSA MAKAZI

       Wakazi wa Kiangu na Chuno mjini Mtwara wamelazimika kuyahama makazi yao baada ya mvua kunyesha na kusababisha kujawa na maji.
        Mvua hiyo ilinyesha usiku wa kuamkia siku ya Jumamosi ya  Desemba 9,2017 saa nane usiku bila kukata mpaka saa kumi na moja jioni. Mvua ilikata kwa muda na kuendelea kunyesha usiku hadi leo Jumapili Desemba 10,2017.Miongoni mwa mali zilizoharibika ni pamoja na magodoro, samani, majokofu na Luninga.Juhudi za kuokoa mali zimefanywa na vijana wa maeneo hayo.
     Aidha wananchi wameiomba Serikali kujenga miundombinu imara ili kuwaepusha na maafa ambayo yamekuwa yakijirudia mara kwa mara pindi mvua kubwa inaponyesha.
      Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA), Desemba 8,2017 ilitoa taarifa kwa umma ikieleza kuwapo vipindi vya mvua kubwa katika  maeneo ya ukanda wa Pwani na kuwataka wananchi kuchuka tahadhari na mvua hizo.

No comments