Header Ads

Serikali ncini Nigeria yaomba radhi suala la utekwaji wa wasichana

Wasichana wa Chibok waliotekwa na Boko Haram

Kwa mujibu wa sirika la BBC limeeleza kuwa kumekuwa na ongezeko la hali ya hasira kwa wazazi wa wasichana wanaodaiwa kutekwa na kundi la wapiganaji wa Boko Haram ambao siku ya jumatatu wamevamia shule moja ya wasichana katika mji wa Daptch nchini humo.
Wazazi wa wanafunzi hao waliokuwa waliokuwa bweni shule Dapchi wamesema kuwa hadi sasa hawaelewi mahala walipo watoto wao.
Serikali ya Nigeria imetoa kauli ya kuomba radhi kwa taarifa zisizo sahihi zilizotolewa siku ya jumatano kwamba baadhi ya wanafunzi waliokolewa na vikosi vya serikali wakati si kweli.
Makundi ya wanaharakati nchini Nigeria yameitaka serikali kutoa orodha ya majina ya wasichana hao waliotekwa ili kuweza kujua idadi yao kamili.
Tukio kama hilo nchini Nigeria lilitokea mwaka 2014 ambapo wasichana 276 wa Chibok walitekwa na Boko Haram.

No comments