Header Ads

TAIWAN YAKUMBWA NA TETEMEKO LA ARDHI

Kutoka Hualen nchini Taiwan watu wanne wameripotiwa kufariki na wengine wamekwama katika majengo baada ya tetemeko la ardhi  kuikumba nchi hiyo katika mji wa Hualien, Taiwan.Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini humo majengo matano yanaripotiwa kuharibika vibaya na yapo katika hatari ya kuanguka, huku watu zaidi ya 140 hawajafikiwa na waokoaji lakini juhudi za uokoaji zikiwa zinaendelea.
Shirika la Habari la Taiwan limeripoti kuwa tetemeko hilo limetokea siku ya Jumanne usiku wa manane na  kujeruhi watu 225 na kuacha majengo yameharibika na juhudi za uokoaji zikiendelea.

No comments