Header Ads

WATU 21 WANUSURIKA KWA AJALI YA TRENI UVINZA


Treni ya abiria ya Shirika la Reli Tanzania iliyokuwa ikitokea mkoani Dodoma kwenda Kigoma imepata ajali katika eneo la Kijiji cha Mpeta wilayani Uvinza.
Ajali hiyo imesababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na kusababisha mabehewa mawili kuanguka katika dimbwi dogo la maji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Martin Othieno amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo. Mpaka sasa hakuna taarifa ya vifo wala idadi ya majeruhi.
Behewa kadhaa bado zimesalia kwenye njia yake baada ya ajali
Naye Kaimu meneja wa wamawasiliano wa Shirika la Reli la Tanzania (TRL) Mohamed Mapondela ameambia BBC kwamba watu watatu wamejeruhiwa.
"Sababu ya ajali bado haijafahamika lakini, timu ya kutathmini ajali iko njiani kuelekea eneo la tukio," amesema.
Ajali ilitokea majira ya saa saba na dakika hamsini mchana eneo la katikati ya stesheni ya Malagarasi na Uvinza.
"Tathmini kamili ya ajali itatolewa pale ambapo mabehewa yatakuwa yameinuliwa."
Bw Mapondela amesema eneo hilo si kwamba ni baya na halina historia ya kupata ajali yoyote ile, ndio maana ni vigumu kusema nini hasa kinaweza kuwa chanzo cha ajali.

No comments