Header Ads

HISTORIA YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HII HAPA

Na Paschal D.Lucas

Nikufahamishe juu ya Historia ya maadhimisho ya mwanamke Duniani kuwa,
Kihistoria, siku hiyo ilianza kwanza kwa kuitwa siku ya wafanyakazi wanawake ya kimataifa.

Maadhimisho yalianza March 8, 1857 baada ya wafanyakazi katika kiwanda cha nguo jijini New York nchini Marekani kugoma kutokana na mazingira mabaya ya kazi hali hiyo ilipelekea takribani wanawake 129 walipoteza maisha kutokana na moto kiwandani hapo mwaka 1910, nchini Denmark kulifanyika kongamano kuwakumbuka wanawake hao waliofariki na walipitisha kuwa March 8 ya kila mwaka, ifanyike siku ya Wanawake Duniani.

Disemba1977, Baraza Kuu la UN lilipitisha na kutangaza kuadhimisha Siku ya Haki za Wanawake na Amani ya Kimataifa.
Na mpaka sasa sherehe hizi zinaadhimishwa kila mwaka ifikapo Machi 8 ya kila mwaka.
Hiyo ndiyo historia fupi ya siku ya mwanamke duniani.

No comments