Header Ads

MWAKYEMBE ATAJA WIZARA,MIKOA NA HALMASHAURI ZINAZOFANYA VIBAYA

Waziri wa Habari sanaa na michezo Mh.Harison Mwakyembe amewataka maafisa habari wa mikoa na wilaya nchini kuwajibika na kutogeukia kuwa nataaluma nyingine bali wawajibike katika kutekeleza majukumu yao ya kiuandishi wa habari na si vinginevyo.
Ametoa agizo hilo wakati akifungua kikao cha siku  tano cha chama cha maafisa mawasiliano serikalini(tagco) kinachojumlisha maafisa habari wa mkoa, wilaya, mashirika na makampuni nchini kilichofanyika katika ukumbi wa AICC mkoani Arusha.
Ametaja Mikoa inayofanya vizuri katika utoaji wa habari kuwa ni Mwanza, Mara, Kagera,Shinyanga,Tabora, Simiyu,Arusha,Tanga,Lindi, Mtwara,Ruvuma, Rukwa,Mbeya , Iringa,Morogoro,Geita,Katavi na Songwe.
Aidha amezitaja Halmashauri tisa nchini zinazofanya vizuri katika kutoa taarifa kwa umma kuwa ni pamoja na Kishapu,Mikindani,Mufindi, Mulele,Katavi,Kinondoni, Ilala,Ubungo na Kibaha.
Kwa upande wa wizara Mh.Mwakyembe amesema katika wizara zote nchini ni wizara  tatu tu ambazo hazina wala hazitoi taarifa zake kabisa katika maendeleo kwa wananchi  na kusema hatazitaja  bali atapeleka majina yake kwa waziri mkuu.

JIONEE VIDEO HAPA CHINI NA USUBSCRIBE


No comments