MWAKYEMBE AWAONYA MAAFISA HABARI, ATAJA MIKOA NA HALMASHAURI ZINAZOFANYA VIBAYA.
Na Paschal
D.Lucas
paschad.lucas@gmail.com
Waziri wa Habari sanaa na michezo Mh.Harison Mwakyembe
amewataka maafisa habari wa mikoa na wilaya nchini kuwajibika na kutogeukia
kuwa nataaluma nyingine bali wawajibike katika kutekeleza majukumu yao ya
kiuandishi wa habari na si vinginevyo.
Ametoa agizo hilo wakati akifungua kikao cha siku tano cha chama cha maafisa mawasiliano
serikalini(tagco) kinachojumlisha maafisa habari wa mkoa, wilaya, mashirika na
makampuni nchini kilichofanyika katika ukumbi wa AICC mkoani Arusha.
Ametaja Mikoa inayofanya vizuri katika utoaji wa habari
kuwa ni Mwanza, Mara, Kagera,Shinyanga,Tabora, Simiyu,Arusha,Tanga,Lindi,
Mtwara,Ruvuma, Rukwa,Mbeya , Iringa,Morogoro,Geita,Katavi na Songwe.
Aidha amezitaja Halmashauri tisa nchini zinazofanya
vizuri katika kutoa taarifa kwa umma kuwa ni pamoja na
Kishapu,Mikindani,Mufindi, Mulele,Katavi,Kinondoni, Ilala,Ubungo na Kibaha.
Kwa upande wa wizara Mh.Mwakyembe amesema katika wizara
zote nchini ni wizara tatu tu ambazo
hazina wala hazitoi taarifa zake kabisa katika maendeleo kwa wananchi na kusema hatazitaja bali atapeleka majina yake kwa waziri mkuu.
Naye Paschal
Shelutete ambaye ni mwenyekiti wa
TALGCO akitoa kwa ufupi maelezo kuhusu
madhumuni ya TALCO kuwa ni kuwaunganisha maafisa habari nchini, kulinda na
kukuza maadili kwa maafisa habari nchini kwa kufuata uandilifu katika
utekelezaji wa majukumu yao katika utoaji wa habari na taarifa kwa uuma.
Kwa upande wake Alvaro Rodriguez ambaye ni mwakilishi Mkazi
wa Umoja wa mataifa nchini amesema kuwa kama umoja wa mataifa maafikiano yatayofanyika kwenye kikao hicho yataleta tija
mabadiliko makubwa kwa Tanzania.
Akitoa neon la shukrani Mkurugenzi Mtendaji wa Habari
maelezo Dr.Hassan Abbasi amewataka wanahabari kuwa na juhudi katika utoaji wa
habari na kuenenda kimkakati,kwa kutoa taarifa fupi zenye maana,
kujituma,kujiongeza na kuwa naubunifu.
Kikao hicho cha TAGBO kitadumu kwa muda wa siku tano
mkoani Arusha ambacho kitajadili masuala ya habari nchini huku kikijivunia kwa
kuzindua tovuti yake ya chama iliyozinduliwa na waziri wa habari Dr.Harrison
Mwakyembe wakati akifungua kikao hicho..
No comments