Header Ads

Sababu iliyomfanya Kamusoko ajifunze Kiswahili

Jambo ambalo hutakiwi kufanya ni ‘kumteta’ Thabani Kamusoko kwa lugha ya Kiswahili ukiamini ni raia wa kigeni na hatoelewa unachozungumza, utakuwa umefeli jamaa ni anatwanga kiswahili hadi cha mtaani.
Kiungo huyo wa Yanga toka Zimbabwe anapozungumza Kiswahili huwezi kujua kama si raia wa Tanzania, Kamusoko yupo vizuri kwa Kiswahili asikwambie mtu.
Wakati anafanya mahojiano na Yahaya Mohamed ‘Mkazuzu’ mjini Morogoro ambako Yanga iliweka kambi kujiandaa na mchezo wake wa kimataifa dhidi ya Wolaitta Dicha, alisema hakuna mwalimu aliyekuwa akimfundisha bali aliamua tu mwenyewe kujifunza Kiswahili.
Katika mazungumzo hayo, Kamusoko akafunguka sababu kubwa iliyomfanyabaamue kujifunza Kiswahili, kumbe ni ishu ya kumrahisishia mawasiliano awapo kazini akisukuma gozi.
“Mpira unahitaji mawasiliano kwa kiasi kikubwa, pia unahitaji kuzungumza lugha moja kwa hiyo niliamua kujifunza Kiswahili ili tuelewane vizuri”-Thabani Scara Kamusoko kiungo Yanga SC.
Hivi karibuni Method Mwanjale ni mchezaji mwingine ambaye anatoka Zimbabwe aliyekuwa anazungumza Kiswahili kwa ufasaha ukiachana na akina Niyonzima, Tambwe, Mavugo ambao nchi zao zinazungumza pia Kiswahili
Credit: SHAFFIHDAUDA.CO.TZ

No comments